Bao
hilo ambalo alifunga jana huko Ujerumani lilimfanya Ronaldo amalize
ukame wake wa kutofunga katika Mechi 3 za Real zilizopita.
Hivi sasa Ronaldo, Messi na Raul wote wamefunga Bao 76 kila mmoja katika Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya.
Akiongea na Canal Plus, Ancelotti alisema: “Ronaldo amerudi. Amefunga, ametengeneza Bao, alifanya vyema!”
Bao la Pili la Real walipoifunga Schalke 2-0 lilifungwa na Mbrazil Marcelo baada ya kazi kubwa ya Ronaldo.
Ancelotti, ambae ndie aliiongoza Real Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI ukiwa ni Ubingwa wao wa 10 Barani Ulaya, wenyewe wanauita ‘Decima’, alishangilia sana Bao la Marcelo na kudiriki kuingia hadi ndani ya Uwanja.
Ancelotti alieleza kwanini alifurahia Bao hilo: “Nilisheherekea Bao lile ndani Uwanjani kwa sababu si kitu cha kawaida kumwona Marcelo akifunga kwa Mguu wake wa Kulia!”
Real Madrid na Schalke zitarudiana hapo Machi 10 huko Santiago Bernabeu Mjini Madrid na Mshindi atatinga Robo Fainali.
Cristiano Ronaldo akikabwa na Wachezaji wawili wa Schalke 04Kikosi Cha Real Madrid kilichoanza jana dhidi ya Schalke 04

No comments:
Post a Comment